Loading...

?Sisi ni nani


 Chuo cha Elimu cha Sanad ni lango la kielimu la kidijitali la Dar al-Mustafa mjini Tarim kwa masomo ya Kiislamu. Hutoa mtaala wa kati wa kielimu, kitarbiyah na kida‘wa wa Dar al-Mustafa Tarim, kwa mtazamo unaounganisha uhalisia wa mapokeo yenye isnadi thabiti na zama za kidijitali.

Chuo hiki kinasimama juu ya uaminifu wa kielimu ulio imara, unaopata nguvu zake kutoka katika isnadi iliyoendelea bila kukatika; ambapo elimu za Sharia Tukufu na zana zake hupokelewa kutoka kwa masheikh na walimu waliopokea elimu yao kutoka kwa wanazuoni wakubwa waliothibiti katika elimu, ndani ya mnyororo wa kielimu unaoendelea hadi kwa Mtume wetu Muhammad( s. w), pamoja na Aali zake na Maswahaba zake.

Kupitia programu za kielimu zilizo na ngazi mbalimbali zinazochanganya elimu, mwenendo na da‘wa, Chuo cha Sanad humwezesha mwanafunzi  popote alipokuwa duniani kuunganishwa na urithi wa Unabii, na kupokea mtaala wa kielimu, kitarbiyah na kida‘wa wa Dar al-Mustafa Tarim kwa mtindo wa kisasa wa kitaaluma unaokuza maarifa, kutakasa nafsi na .kuitumikia dini na Umma

ujumbe

Ili kuchangia katika kuitumikia Sharia Tukufu, na kutekeleza wajibu wa kueneza urithi mtukufu wa Unabii, ambao hauwezi kuhifadhiwa wala kutekelezwa ipasavyo isipokuwa kupitia watu waliobobea na kuhitimu kwa ajili yake. Hili hufanyika kupitia: (kupandikiza urithi wa Unabii ndani ya nafsi zitakazoueneza).

dira

Kufikia uongozi katika nyanja ya elimu ya kielektroniki yenye malengo ya kheri, na liwe Chuo cha Sanad lango la kwanza kwa wanaotamani kupokea elimu yenye isnadi iliyo ya wastani kwa Ahli -Sunna wal-Jamaa (mtaala wa kielimu, kimaadili na kida‘wa wa Dar al-Mustafa Tarim kwa masomo ya Kiislamu).

malengo


Kufundisha elimu za Sharia kwa isnadi iliyoendelea kwa usahihi na kwa njia ya urithi wa kielimu, sambamba na kutumia mbinu na njia za kisasa zenye manufaa na kuunganisha elimu na uhalisia ili kurahisisha utekelezaji.

Kuzitakasa nafsi kwa ikhlasi ya nia, kuitakasa mioyo na kuendeleza maadili mema.

Kukuza ndani ya nyoyo utukufu wa wito wa kumlingania Mwenyezi Mungu na kutekeleza wajibu wake, pamoja na kuimarisha uwezo na juhudi katika maelezo mazuri na kufikisha kheri kwa wigo mpana iwezekanavyo.

Kunufaika na njia za kisasa katika kurahisisha kupokea elimu kutoka kwa wanazuoni na kuhifadhi urithi wao wa kielimu, pamoja na kupokea mtaala wa Dar al-Mustafa – Tarim kwa masomo ya Kiislamu kwa wale wasioweza kufika chuoni au kujitolea kikamilifu kwa masomo, yote hayo kwa mujibu wa maono na mbinu ya kielimu iliyo wazi.