Loading...

Mpango huu unawalenga Waislamu kwa ujumla wanaotaka kujipatia elimu ya kisharia ya wajibu, na yale yanayojulikana wazi katika dini kwa msururu wa masomo yenye sanad ulioungana. Mpango huu unajumuisha idadi ya masomo yanayowasilishwa kwa mbinu za kielimu zilizo thabiti na kwa njia iliyorahisishwa, Masomo yake yako wazi bila kuwekewa muda maalumu; hivyo mwanafunzi anaweza kujisajili, kusoma masomo, na kuyakamilisha kwa wakati na muda anaoona unamfaa.

Video ya utangulizi wa programu

Jinsi ya kusoma

Programu ina ngazi moja tu, yenye kozi tatu. ngazi ya kwanza itakuwa kwa lugha ya kiswahili kisha ngazi nyingine zitakuwa kwa lugha ya kiarabu kwa anae taka kujiendeleza lazima ajue kiarabu, Mwanafunzi akipata kiwango cha ufaulu kisichopungua asilimia 70% katika vitabu vilivyowekwa, atapewa cheti cha kukamilisha programu.

Masomo yako wazi muda wote bila kujifunga na muda maalumu. Mwanafunzi anaweza kusoma wakati wowote anapoona inafaa.

 Akifungua akaunti, mwanafunzi anaweza kuanza moja kwa moja kusoma masomo yote yaliyopo, na kuyatazama wakati wowote. Akimaliza kitabu, anaweza kufanya mtihani na kuendelea na kingine

Akipata angalau 70% katika kila kitabu, anapewa cheti cha kukamilisha programu.

  • Mtihani wa somo: Mtihani wa maswali ya kuchagua (chagua jibu sahihi) baada ya kila somo, na kiwango cha ufaulu ni asilimia 80%.
  • Hakuna mitihani ya kila mwezi au ya nusu muhula, isipokuwa mtihani wa mwisho tu kwa kila kitabu. Hii ni mitihani ya kielektroniki, ambapo kuna dirisha maalumu lililo baada ya somo la mwisho la kila kitabu. Mwanafunzi akimaliza kusoma masomo ya kitabu kilichopangwa, anaweza kufanya mtihani wakati wowote unaomfaa, na matokeo pamoja na cheti hutumwa kwake mara moja